Thursday, December 18, 2014

MWONGOZO WA KUANDIKA KATIBA YA KIKUNDI


FOMATI YA KUANDAA KATIBA  ZA VIKUNDI

SEHEMU YA KWANZA
1.       UTANGULIZI

Sehemu hii huonyesha  jina la kikundi, mahali kitakapofanyia shughuli zake na nafasi ya kikundi kama kitakuwa cha kisiasa, kujiinua kiuchumi, hakitafungamana na chama au imani yoyote na haina ya shughuli zitakazofanywa na kikundi.
SEHEMU YA PILI
2.       DIRA, LENGO KUU, MALENGO MAHUSUSI YA KIKUNDI NA SHUGHULI ZA KIKUNDI

Katika sehemu hii kikundi hufafanua na kujipambanua kuhusu malengo ya kikundi.

·         Dira ni  ndoto za kikundi kwa baadae .Ni maono ya kikundi kwa baadae katika kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wanachama.

·         Lengo kuu ni kile ambacho kikundi  kinataka kufikia na ili kufikia lengo kuu lazima kuwepo na malengo mahususi yanayopelekea kufikiwa kwa lengo kuu.

·         Malengo mahususi : ni  mambo ambayo yanatarajiwa kufikiwa kutokana na shughuli zilizopangwa ili kufikia lengo kuu. Malengo mahususi huwa ni mwongozo wa tathimini kuhusu mwelekeo wa kikundi.

·         Shughuli : ni mambo ambayo utekelezwa na wanakikundi ili kuweza kufikia malengo mahususi hatimaye kufikia lengo kuu. Utekelezaji wa shughuli ndani ya kikundi hutegemea malengo mahususi ambayo kikundi kimejiwekea.
SEHEMU YA TATU
3.       UANACHAMA , HAKI NA WAJIBU WA MWANAKIKUNDI

·         Katika sehemu hii kikundi hubainisha taratibu za kujiunga na kikundi, sifa za mwanakikundi na ukomo wa uanachama.

·         Pia katika shemu hii haki na wajibu wa mwanachama huonyeshwa.
SEHEMU YA NNE
4.       USIMAMIZI WA MAPATO NA MALI NYINGINE ZA KIKUNDI

·         Usimamizi wa fedha za kikundi huwekwa wazi ili kuondoa migongano ambayo inaweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kikundi.

·         Kwenye katiba inaweza kuandikwa kuwa  kikundi kitakuwa na akaunti maalumu ambayoitatumia jina la kikundi na aina ya benki itategemea maamuzi ya wanakikundi kupitia mkutano mkuu.

·         Pia kikundi  huchagua watia saini wanne ambao hutoka kwenye makundi mawili. Kundi A huwa na watu wawili kutoka upande wa uongozi na kundi B huwa na wajumbe wawili ambao hawana nafasi ya uongozi kwenye kikundi.
SEHEMU YA TANO
5.       UONGOZI NA USIMAMIZI WA KIKUNDI

·         Nafasi za uongozi katika kikundi ni mwenyekiti, mwenyekiti msaidizi, katibu na mweka hazina

·         Sifa na majukumu  ya  kila kiongozi yaanishwe ili wanakikundi waweze kuchagua kiongozi atakayesimamia vema kikundi. Katika hili wanakikundi wahakikishe wanachagua viongozi kwa kufuata sifa walizoanisha pasiwepo na upendeleo wowote kwani wasipofanya hivi kikundi kitasambaratika kwa muda mfupi.

·         Wanakikundi waanishe uchaguzi wa viongozi utafanyika baada ya mda gani kwa vipindi vingapi

·         Wanakiundi waainishe mambo mengine wanayofikiri  yatasaidia kikundi katika kipengere cha viongozi

·         Idadi ya wajumbe au wanakikundi watakaopiga kura.

·         Kamati mbalimbali.
SEHEMU YA SITA
6.       MIKUTANO YA KIKUNDI

·         Kuna  mikutano ya aina tatu

 

Ø  Mkutano mkuu wa mwaka unaofanyika mwishoni mwa mwaka kutegemea na mwisho wa mwaka wa kikundi kutegemea mapendekezo ya wanakikundi.

Ø  Mkutano wa kawaida huu utategemea pia makubaliano yawanakikundi mf. Yaweza kuwa kwa wiki mara moja, kwa mwezi mara moja au kwa miezi mitatu mara moja.

Ø  Mkutano wa dharura mkutano huu unategemea dharura itakayojitokeza  miongoni mwa wanakikundi na unaweza kuitishwa wakati wowote kutegemea umuhimu wa jambo husika.

·         Wajumbe wa mikutano hii ni wanakikundi  wa kikundi husika

·         Maamuzi ya mkutano yatakua sahihi endapo yatakubaliwa na nusu ya wanakikundi  na zaidi.
SEHEMU YA SABA
7.       MICHANGO NA MAPATO YA KIKUNDI

·         Kuna vyanzo tofauti  vya mapato ya kikundi

a.       Michango ya kila mwezi au wiki kutegemea  makubaliano ya mkutano mkuu.

b.      Faini kutoka kwa wanakikundi wanaokiuka taratibu kama kuchelewa au kutohudhuria  kwenye mkutano.

c.       Misaada kwa wadau mbalimbali wenye  nia njema na kikuu.
SEHEMU YA NANE
8.       MEREKEBISHO YA KATIBA

·         Katika uandishi wa katiba ya kikundi ni vyema kuwepo kipengele  kinachoruhusu marekebisho ya katiba pale inapobidi. Misingi yakubadilisha kipengele chochote lazima iwekwe vizuri ili iweze kufahamika kwa kika mwanakikundi.  Mfano kinaweza kuandikwa; Kifungu chochote kinaweza kufanyiwa marekebisho  kwa kutegemea maamuzi ya mkutano mkuu na hoja ya mabadiliko itatoka kwa mtu ambaye ni mwanakikundi hai.
SEHEMU YA TISA
9.       KUVUNJIKA KWA KIKUNDI

·         Mara nyingi  lengo la kikundi ni kuwa endelevu, kwa hiyo kwenye katiba ni vizuri kuandikwa kwa hivi, kikundi hakitavunjika isipokuwa  kwa sababu ya msingi au kama ni agizo la sheria za nchi.
        ·         Endapo kikundi kitavunjwa mali zote na madeni ya kikundi yatagawiwa kwa wanakikundi
                wote.
SEHEMU YA  TISA
10. KUPITISHWA KWA  KATIBA

·         Katiba hii ya kikundi cha ……………….. ya mwaka imepitishwa siku ya tarehe ……….mwezi wa …… mwaka  na wajumbe ambao majina na sahihi zao zinaonekana  chini.

 

Sahihi…………………..                                                             Sahihi  ………………….

Jina la mwenyekiti…………                                                  Jina la katibu…………….

MWENYEKITI                                                                        KATIBU

 
ORODHA YA MAJINA YA WAJUMBE WALIOPITISHA KATIBA YA KIKUNDI CHA …………….

S/N
JINA
CHEO
SAHIHI
1.
 
 
 
2.
 
 
 
3.
 
 
 
4.
 
 
 
5.
 
 
 
6.
 
 
 
7.
 
 
 
8.
 
 
 
9.
 
 
 
10.
 
 
 
11.
 
 
 
12.
 
 
 
13.
 
 
 
14.
 
 
 
15.
 
 
 
16.
 
 
 
17.
 
 
 
18.
 
 
 
19.
 
 
 
20.
 
 
 
21.
 
 
 

 

 Imeandaliwa na
Godfrey Vedasto.
 

 

 

 

 

 

 

 

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | LunarPages Coupon Code