FOMATI YA KUANDAA KATIBA ZA
VIKUNDI
SEHEMU YA KWANZA
1. UTANGULIZI
Sehemu hii huonyesha
jina la kikundi, mahali kitakapofanyia shughuli zake na nafasi ya
kikundi kama kitakuwa cha kisiasa, kujiinua kiuchumi, hakitafungamana na chama
au imani yoyote na haina ya shughuli zitakazofanywa na kikundi.
SEHEMU YA PILI
2. DIRA, LENGO KUU, MALENGO MAHUSUSI YA
KIKUNDI NA SHUGHULI ZA KIKUNDI
Katika sehemu hii kikundi hufafanua na kujipambanua kuhusu
malengo ya kikundi.
·
Dira ni
ndoto za kikundi kwa baadae .Ni maono ya kikundi kwa baadae katika
kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wanachama.
·
Lengo kuu ni kile ambacho kikundi kinataka kufikia na ili kufikia lengo kuu
lazima kuwepo na malengo mahususi yanayopelekea kufikiwa kwa lengo kuu.
·
Malengo mahususi : ni mambo ambayo yanatarajiwa kufikiwa kutokana
na shughuli zilizopangwa ili kufikia lengo kuu. Malengo mahususi huwa ni
mwongozo wa tathimini kuhusu mwelekeo wa kikundi.
·
Shughuli : ni mambo ambayo utekelezwa na
wanakikundi ili kuweza kufikia malengo mahususi hatimaye kufikia lengo kuu.
Utekelezaji wa shughuli ndani ya kikundi hutegemea malengo mahususi ambayo
kikundi kimejiwekea.
SEHEMU YA TATU
3. UANACHAMA , HAKI NA WAJIBU WA MWANAKIKUNDI
·
Katika sehemu hii kikundi hubainisha taratibu za
kujiunga na kikundi, sifa za mwanakikundi na ukomo wa uanachama.
·
Pia katika shemu hii haki na wajibu wa
mwanachama huonyeshwa.
SEHEMU YA NNE
4. USIMAMIZI WA MAPATO NA MALI NYINGINE ZA
KIKUNDI
·
Usimamizi wa fedha za kikundi huwekwa wazi ili
kuondoa migongano ambayo inaweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu
ya kikundi.
·
Kwenye katiba inaweza kuandikwa kuwa kikundi kitakuwa na akaunti maalumu
ambayoitatumia jina la kikundi na aina ya benki itategemea maamuzi ya
wanakikundi kupitia mkutano mkuu.
·
Pia kikundi
huchagua watia saini wanne ambao hutoka kwenye makundi mawili. Kundi A
huwa na watu wawili kutoka upande wa uongozi na kundi B huwa na wajumbe wawili
ambao hawana nafasi ya uongozi kwenye kikundi.
SEHEMU YA TANO
5. UONGOZI NA USIMAMIZI WA KIKUNDI
·
Nafasi za uongozi katika kikundi ni mwenyekiti,
mwenyekiti msaidizi, katibu na mweka hazina
·
Sifa na majukumu ya kila
kiongozi yaanishwe ili wanakikundi waweze kuchagua kiongozi atakayesimamia vema
kikundi. Katika hili wanakikundi wahakikishe wanachagua viongozi kwa kufuata
sifa walizoanisha pasiwepo na upendeleo wowote kwani wasipofanya hivi kikundi
kitasambaratika kwa muda mfupi.
·
Wanakikundi waanishe uchaguzi wa viongozi
utafanyika baada ya mda gani kwa vipindi vingapi
·
Wanakiundi waainishe mambo mengine
wanayofikiri yatasaidia kikundi katika
kipengere cha viongozi
·
Idadi ya wajumbe au wanakikundi watakaopiga
kura.
·
Kamati mbalimbali.
SEHEMU YA SITA
6. MIKUTANO YA KIKUNDI
·
Kuna mikutano ya aina tatu
Ø
Mkutano mkuu wa mwaka unaofanyika mwishoni mwa
mwaka kutegemea na mwisho wa mwaka wa kikundi kutegemea mapendekezo ya
wanakikundi.
Ø
Mkutano wa kawaida huu utategemea pia
makubaliano yawanakikundi mf. Yaweza kuwa kwa wiki mara moja, kwa mwezi mara
moja au kwa miezi mitatu mara moja.
Ø
Mkutano wa dharura mkutano huu unategemea
dharura itakayojitokeza miongoni mwa
wanakikundi na unaweza kuitishwa wakati wowote kutegemea umuhimu wa jambo
husika.
·
Wajumbe wa mikutano hii ni wanakikundi wa kikundi husika
·
Maamuzi ya mkutano yatakua sahihi endapo
yatakubaliwa na nusu ya wanakikundi na
zaidi.
SEHEMU YA SABA
7. MICHANGO NA MAPATO YA KIKUNDI
·
Kuna vyanzo tofauti vya mapato ya kikundi
a.
Michango ya kila mwezi au wiki kutegemea makubaliano ya mkutano mkuu.
b.
Faini kutoka kwa wanakikundi wanaokiuka taratibu
kama kuchelewa au kutohudhuria kwenye
mkutano.
c.
Misaada kwa wadau mbalimbali wenye nia njema na kikuu.
SEHEMU YA NANE
8. MEREKEBISHO YA KATIBA
·
Katika uandishi wa katiba ya kikundi ni vyema
kuwepo kipengele kinachoruhusu
marekebisho ya katiba pale inapobidi. Misingi yakubadilisha kipengele chochote lazima
iwekwe vizuri ili iweze kufahamika kwa kika mwanakikundi. Mfano kinaweza kuandikwa; Kifungu chochote
kinaweza kufanyiwa marekebisho kwa
kutegemea maamuzi ya mkutano mkuu na hoja ya mabadiliko itatoka kwa mtu ambaye
ni mwanakikundi hai.
SEHEMU YA TISA
9. KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
·
Mara nyingi
lengo la kikundi ni kuwa endelevu, kwa hiyo kwenye katiba ni vizuri
kuandikwa kwa hivi, kikundi hakitavunjika isipokuwa kwa sababu ya msingi au kama ni agizo la
sheria za nchi.
·
Endapo kikundi kitavunjwa mali zote na madeni ya
kikundi yatagawiwa kwa wanakikundi wote.
SEHEMU YA TISA
10. KUPITISHWA KWA KATIBA
·
Katiba hii ya kikundi cha ……………….. ya mwaka
imepitishwa siku ya tarehe ……….mwezi wa …… mwaka na wajumbe ambao majina na sahihi zao
zinaonekana chini.
Sahihi………………….. Sahihi ………………….
Jina
la mwenyekiti…………
Jina la katibu…………….
MWENYEKITI KATIBU
S/N
|
JINA
|
CHEO
|
SAHIHI
|
1.
|
|
|
|
2.
|
|
|
|
3.
|
|
|
|
4.
|
|
|
|
5.
|
|
|
|
6.
|
|
|
|
7.
|
|
|
|
8.
|
|
|
|
9.
|
|
|
|
10.
|
|
|
|
11.
|
|
|
|
12.
|
|
|
|
13.
|
|
|
|
14.
|
|
|
|
15.
|
|
|
|
16.
|
|
|
|
17.
|
|
|
|
18.
|
|
|
|
19.
|
|
|
|
20.
|
|
|
|
21.
|
|
|
|
30 comments:
Mr Godfrey hongera san kwa kuandika muongozo mzuri wa katiba ya kikundi asante san. Najua vikundi vingi vinkufa sababu havina katiba ya kuongoza kikundi ila nimejiufunza sana
Hongera ndugu
Shukran sana kiongoz kwa muongozo wako naimani nitafanikiwa lengo langu
Da!imekaa njema sana
Asante sana kaka imenisaidia kuandaa katiba ya kikundi chetu cha wana familia
Hongera mkuu...imekaa poa sana ii...
Ubarikiwe mana umetupa mwongozo uliosahihi!
Dah ! safi sana. Maana sikuweza kufika hapa isipokuwa ni kwa sababu nilikuwa nikitafuta muongozo wa aina hii.
Dah ! Hapa sasa napumua. Uongozi bila muongozo kweli ni mzigo. Kuanzia hapa sasa naupunguza mzigo.
Hongera Ndugu. tuletee mengine zaidi juu ya vikundi.
Thanks Ndio niko najaribu kuandika
Shukulan sana kwa mwongozo wako
Thanks Brooh..
Soo much to learn in here.
Safi sana na imenisaidia kwakweli
Hongera sana nimefurahi kupata mwongozo huu asante ndugu
Asante kwa muongozo mzur
is it an approved format by the Gvt of Tanzania
Hasante Sana umetoa Mwongozo mzuri wa uhandishi wa katiba
Ahsante sana umetoa muongozo mzuri
Asante
Asante
Hongera Sana Kaka ,tushaanza kunufaika nayo ,shukrani
imekaa powa sana
Ubarikiwe sana kwa maono haya
hongera kujana kwa kutupatia muongozo mzuri wa katiba za vikundi🙏
hongera kujana kwa kutupatia muongozo mzuri wa katiba za vikundi🙏
Asante sanaaaa kiongozi kwa mwingozo mzuri sana natumai utamfaa kila mtu atakayeufuata
Safi sana
Safi Sana kaka,
good sample
Muongozo huu umepangwa vizuri na napendekeza watu wautumie utawasaidia sana.shukrani mwandaaji ubarikiwe.
Asante kwa muongozo
Post a Comment